Rais wa Ukraine Volodymr Zelensky kukutana na Trump Jumatatu
16 Agosti 2025Matangazo
Zelensky amesema alifanya mazungumzo ya muda mrefu na Trump leo baada ya kiongozi huyo wa Marekani kukutana na Putin huko Alaska. Alimshukuru Trump kwa mwaliko wa kukutana naye ana kwa ana mjini Washington siku ya Jumatatu na kuongeza kuwa watajadili masuala yote ya kukomesha mauaji na vita.
Ukraine, Ulaya wana matumaini na mkutano wa Trump na Putin
Zelensky alisisitiza umuhimu wa kuyahusisha mataifa ya Ulaya katika mazungumzo hayo ya amani.
Amesema ni muhimu kwa mataifa hayo kuhusika katika kila hatua ili kuhakikisha kuwepo kwa dhamana za usalama pamoja na Marekani.
Baada ya mazungumzo hayo na Trump, Zelensky pia alifanya mazungumzo na viongozi wengine wa Ulaya kwa njia ya simu.