Rais Samia aipongeza Simba kusonga mbele kombe la Shirikisho
28 Aprili 2025Matangazo
Rais Samia amesema Simba imeipatia Tanzania heshima kubwa, huku akiitakia kila la kheri na kusema ataiunga mkono klabu hiyo wakati wote.
Katika hatua ya nusu fainali siku ya Jumapili mjini Durban, Simba ilitoka sare ya 0-0 na klabu ya Stellenbosch ya Afrika Kusini na kufuzu kutokana na ushindi wa 1-0 katika uwanja wa nyumbani.
Simba watamenyana na wababe wa Morocco Renaissance Berkane katika fainali ya ambapo mechi ya awali itachezwa nchini Morocco Mei 17 na mechi ya marudio Mei 25 jijini Dar-Es-Salaam.