Rais wa Syria asema nchi haiunganishwi kwa kumwaga damu
18 Agosti 2025Kiongozi huyo alikuwa akipinga mgawanyiko wowote wa nchi na kuishutumu Israel kwa kuingilia nchi hiyo upande wa kusini.Kiongozi huyo amesikika akisema bado wana vita nyingine mbele yao ya kuunganisha Syria, kupitia aina fulani ya maelewano kwa sababu Syria imechoka na vita.Kauli yake, iliyotangazwa leo kupitia televisheni ya taifa inatolewa wakati mamia ya watu walikuwa wakiandamana katika mkoa wa Sweida kusini mwa Syria, wakilaani ghasia za kimadhehebu zilizotokea mwezi uliopita na kudai haki ya kujitawala kwa mkoa huo unaokaliwa na watu wengi wa madhehebu ya Druze.Katika maandamano ya Sweida, baadhi ya waandamanaji walipeperusha bendera ya Israel na kudai haki ya kujitawala kwa mkoa huo. Wiki ya umwagaji damu ilianza Julai 13 kwa mapigano kati ya Wadruze na Wabedui wa Kisunni, na hali ikazidi kuwa mbaya kwa kuhusisha vikosi vya serikali, huku Israel ikifanya mashambulizi pia.