Rais wa Syria aionya Israel dhidi ya kuiburuza Syria vitani
17 Julai 2025Katika hotuba iliyorushwa mapema alfajiri katika runinga ya taifa, rais wa Syria Ahmed al-Sharaa amesema hawatawapa Israel fursa ya kuwaingiza watu wa Syria katika vita ambavyo vinatumika tu kuigawanya nchi na kupanda uharibifu.
Rais huyo wa Syria ameilaumu Isreal kwa kutumia ukosefu wa utulivu kufuatia mabadiliko ya utawala, akiituhumu kwa kuilenga miundombinu ya umma na kutaka kukwamisha juhudi za ujenzi mpya.
Akizungumzia machafuko katika mkoa wa kusini wa Sweida, Al-Sharaa amesema serikali yake imeingilia kati kufikisha mwisho makabiliano kati ya makundi ya eneo hilo yaliyokuwa yakipigana.
Wakati huo huo, China imetoa wito uhuru wa Syria uheshimiwe baada ya Israel kufanya mashambulizi dhidi ya vikosi vya nchi hiyo, ikiwa ni katika kuiunga mkono jamii ya wachache ya Druze.