MigogoroSyria
Rais wa Syria aapa kushughilikia mauaji ya jamii ya Alawite
10 Machi 2025Matangazo
Mauaji hayo yaliibua ukosoaji wa kimataifa dhidi ya ghasia mbaya zaidi tangu kupinduliwa kwa Bashar al-Assad.
Shirika linalofuatilia vita nchini humo la Syrian Observatory for Human Rights limesema kwenye ripoti yake mapema leo kuwa raia 973 wameangamia ama kwa kuuliwa hadharani au kupitia operesheni ya takasatakasa ya kikabila iliyofanywa na maafisa wa usalama au wapiganaji wanaoiunga mkono serikali katika eneo la pwani la jamii ya wachache ya Alawite, anakotokea Assad.
Mkuu wa haki za Binaadamu kwenye Umoja wa Mataifa Volker Turk amesema jana Jumapili kwamba mauaji hayo "lazima yakomeshwe mara moja", huku Umoja wa Nchi za Kiarabu, Umoja wa Mataifa, Marekani, Uingereza na serikali nyingine zikilaani ghasia hizo.