Rais wa Somalia anusurika shambulizi la bomu Mogadishu
19 Machi 2025Bomu lililokuwa limetegwa njiani limelipuka nje ya kasri la rais nchini Somalia jana na serikali kusema kuwa bomu hilo lilikuwa limeulenga msafara wa rais. Taarifa ya wizara ya mawasiliano imekitaja kitendo hicho kuwa cha "uoga." Kundi la kigaidi la wanamgambo wa al-Shabab limedai kuhusika na utegaji wa bomu hilo.Watu 11 wauawa katika shambulizi la kigaidi Mogadishu
Taarifa hiyo haikutaja idadi kamili ya waliofariki kutokana na bomu hilo ila shuhuda mmoja amesema kwamba amehesabu miili mitatu ya watu katika eneo la tukio. Rais wa Somalia amenusurika na shambulizi hilo. Kundi la al-Shabab ambalo linaipinga serikali ya shirikisho la Somalia, hufanya mashambulizi ya mara kwa mara ya mabomu likiwalenga maafisa wa serikali na wanajeshi katika taifa hilo la Pembe ya Afrika.