Kagame aonya makubaliano ya amani na Kongo yasikiukwe
4 Julai 2025Matangazo
Katika mkutano na waandishi wa habari mjini Kigali wa Ijumaa 04.07.2025, Kagame amefafanua zaidi akisema kama kama upande ambao Rwanda inakabiliana nao kwenye makubaliano hayo utawahadaa kwa namna yoyote, watalishughulikia vilivyo tatizo.
Kagame ameitoa kauli hiyo muda mfupi baada ya waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda kusema wanataka mazungumzo zaidi na serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kujadili changamoto ambazo hazikujumuishwa kwenye makubaliano yanayolenga kuumaliza mzozo nchini humo.
Itakumbukwa kuwa M23, hawakushiriki kwenye makubaliano hayo ya amani kati ya nchi hizo.