Rais wa Marekani Donald Trump asitisha ushuru kwa siku 90
10 Aprili 2025Wakati huo huo, Trump amepandisha kiwango cha ushuru kwa China hadi kufikia asilimia 125. Uamuzi wa Trump wa kusitisha ushuru wa kimataifa ulisababisha hofu duniani kote kwa kipindi cha wiki nzima hadi hivi sasa tangu alipotangaza hatua ya kuweka ushuru kwa bidhaa zinazoingizwa nchini Marekani.
Hata hivyo, hatua ya rais huyo wa Marekani imesababisha soko la kimataifa kuzorota. Kutokana na hayo Rais Trump ghafla ameamua kusitisha ushuru kwa mataifa mengi kwa muda wa siku 90, amesema "hatutaki kuziumiza nchi ambazo hazistahili kuumizwa. Na nchi zote hizo zinataka kujadiliana nasi. Tunataka kuzingaUshuru wa Trump waanza kutekelezwatia haki. Ingawa tunazijali nchi hizo, lakini tunapaswa kuijali zaidi nchi yetu.”
Ushuru wa Trump waanza kutekelezwa
Mabadiliko hayo ya Trump, ameyafanya chini ya saa 24 baada ya hatua za ushuru mpya kuanza kufanya kazi kwa washirika wengi wa kibiashara wa Marekani hali ambayo ilisababisha masoko ya hisa kutetereka.
Wakati huo huo, Trump ameiongezea China kiwango cha ushuru hadi kufikia asilimia 125 kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka China na kuingizwa nchini Marekani. Hapo mwanzo alikuwa ameiwekea nchi hiyo ushuru wa asilimia 104 ambayo ulianza kufanya kazi siku ya Jumatano.
Kwa upande wake China imepinga hatua ya Marekani ambayo imesema ni vitisho na usaliti. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Lin Jian, amesema nchi yake ''itapambana hadi mwisho" na kwamba mlango wa China uko wazi kwa mazungumzo, lakini lazima yazingatie kuheshimiana.
Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen, na viongozi wengine wa Ulaya walipokea vyema hatua ya Trump ya hivi punde.
Trump atishia ushuru zaidi kwa China
Von der Leyen ameusifu uamuzi wa Trump wa kusitisha kwa muda ushuru kwa bidhaa mbalimbali zinazoagizwa nje ya Marekani ikiwa ni pamoja na nchi za Ulaya. Hata hivyo, Von der Leyen hakueleza iwapo Ulaya inakusudia kusonga mbele na hatua zake za kuiwekea Marekani ushuru katika hali ya kulipiza kisasi. Trump aliziwekea nchi za Ulaya ushuru wa asilimia 20.
Vyanzo: RTRE/AP