SiasaLebanon
Rais wa Lebanon aitaka Hezbollah kuweka chini silaha
31 Julai 2025Matangazo
Akitoa hotuba ya kuadhimisha Siku ya Jeshi, Aoun amesisitiza dhamira yake ya kutanua mamlaka ya serikali kote nchini Lebanon, kuwapokonya silaha Hezbollah , na kwamba nchi hiyo inahitaji dola bilioni 1 kwa mwaka kwa muda wa miaka 10 ili kusaidia kuliimarisha jeshi na vikosi vya usalama nchini Lebanon.
Kauli ya rais Aoun imetolewa siku moja baada ya kiongozi wa Hezbollah huko Lebanon Sheikh Naim Qassem kusema kuwa wanaodai kupokonywa silaha kwa kundi hilo wanazingatia zaidi malengo ya Israel na kwamba kamwe hawatojisalimisha kwa Israel.