Rais wa Lebanon aenda Saudia akinuia kuimarisha uhusiano
3 Machi 2025Hiyo ni ziara ya kwanza ya Aoun nje ya nchi tangu mkuu huyo wa zamani wa jeshi inayeaminika aliungwa mkono na Saudi Arabia na Marekani kuchaguliwa kuwa rais wa Lebanon mnamo Januari 9.
Kuchaguliwa kwake kulihitimisha miaka miwili ya kukosekana serikali nchini humo katikati ya mzozo wa kisiasa na hali mbaya ya kiuchumi. Inaaminika kudhoofika kwa nguvu za kundi la Hezbollah lililokuwa na ushawishi nchini Lebanon ndiyo kuliwezesha kuchaguliwa kwa Aoun kuwa Rais na mwanadiplomasia wa siku nyingi Nawaf Salam kuwa waziri mkuu.
Akiwa mjini Riyadh, Aoun atakutana na mwanamfalme wa Saudia Arabia Mohammed bin Salman akilenga kufufua mahusiano kati ya nchi hizo mbili hasa kuondolewa vikwazo vya kusafiri na biashara vilivyowekwa na Saudi Arabia dhidi ya Lebanon.