Rais wa kwanza wa Namibia, Sam Nujoma, afariki dunia
9 Februari 2025Rais wa sasa wa Namibia Nangolo Mbumba, ametangaza kifo cha kiongozi huyo aliyepigania uhuru wa Namibia kwenye taarifa kwa taifa siku ya Jumapili. Amesema Sam Nujoma alifariki Jumamosi jioni katika hospitali alikokuwa amelzwa tangu wiki tatu zilizopita. Nujoma alikuwa kiongozi wa Jumuiya ya Watu wa Afrika Kusini na Magharibi, iliyokuwa vuguvugu la ukombozi na baadaye lilikuwa chama tawala cha kwanza wakati Namibia ilipopata uhuru wake kutoka kwa Afrika Kusini. Aliapishwa kama rais wa kwanza wa Namibia tarehe 21 Machi, mwaka1990. Alichaguliwa tena kwa vipindi viwili zaidi vya uongozi mwaka 1994 na 1999. Ameacha mke na watoto wawili. Afrika Kusini ilichukua udhibiti wa nchi Namibia kama sehemu ya Vita vya Kwanza vya Dunia katika ushindi wa kujikomboa kutoka kwa wakoloni ya Wajerumani.