Rais wa Kenya aonya dhidi ya jaribio la kuipindua serikali
9 Julai 2025Matangazo
Rais Ruto amesema kuwa wafadhili wanataka kuanzisha fujo, kuandaa maandamano, kuchoma mali za watu, kuleta maafa ili kuipindua serikali kabla ya mwaka 2027.
Ruto akabiliwa na kibarua cha kudhibiti maandamano na kuwashawishi Gen Z
Haya yanajiri wakati ambapo tume ya haki za binadamu inayofadhiliwa na serikali imesema idadi ya watu waliofariki katika maandamano dhidi ya serikali siku ya Jumatatu imefikia 31, hii ikiwa idadi ya juu zaidi ya vifokwa siku moja tangu maandamano yalipoanza mapema mwaka huu.
Tume hiyo pia imesema watu wengine 107 walijeruhiwa na zaidi ya 500 kukamatwa huku kukiwa na uharibifu mkubwa wa mali.
Idadi ya waliokamatwa inawiana kwa kiasi kikubwa na ile iliyotolewa na polisi.