Rais wa Iran aiamuru nchi hiyo kusitisha uhusiano na IAEA
2 Julai 2025Matangazo
Hatua hii inajiri baada ya bunge la Iran kupitisha sheria inayositisha ushirikiano huo.
Haikuwa wazi hatua hii itamaanisha nini hasa kwa IAEA, ambayo imekuwa ikifuatilia mpango wa nyuklia wa Iran. Shirika hilo hadi sasa halijatoa maoni yoyote kuhusu hatua hiyo.
Baada ya bunge kupitisha uamuzi huo, Baraza la Juu la usalama wa Taifa nchini Iran lilipaswa kufuatilia na kusimamia utekelezwaji wake. Rais Masoud Pezeshkian ni mkuu wa Baraza hilo na amri yake inaashiria muswada huo utatekelezwa.