Rais wa Indonesia: Maandamano 'yanakaribia uhaini na ugaidi'
31 Agosti 2025Maandamano hayo, yaliyoanza kwa kupinga marupurupu ya kifahari kwa wabunge na mishahara midogo, sasa yamegeuka vurugu, yakisababisha vifo vya watu watatu na mashambulizi dhidi ya nyumba za mawaziri na wabunge akiwemo waziri wa fedha Sri Mulyani. Ni Muylani ni mtu mashuhuri ambaye aliwahi kuwa mkurugenzi mkuu wa Benki ya Dunia na amewahi kuwa waziri wa fedha kwa marais watatu tofauti.
Akilihutubia taifa kutoka Ikulu ya Jakarta, Rais wa Indonesia Prabowo Subianto amelaani vitendo hivyo alivyosema vinakurubia kwenye uhaini na ugaidi, na kuaahidi uchunguzi wa kina na msaada kwa familia ya marehemu, huku maandamano yakisambaa katika miji mikuu kote nchini humo. Rais Probowo amesema pia kwamba Bunge limekubali kufuta baadhi ya marupurupu ya wabunge.
Maandamano yameenea katika miji mingine mikubwa, ikiwa ni pamoja na Yogyakarta, Bandung, Semarang na Surabaya huko Java, na Medan katika jimbo la Sumatra Kaskazini.