Afwerki aionya Ethiopia kuhusu kuanzisha vita dhidi yake
20 Julai 2025Eritrea na Ethiopia wamekuwa na mahusiano mabaya tangu Eritrea ilipojinyakulia uhuru wake mwaka 1993 kutoka Ethiopia na wamepigana vita vilivyosababisha mauaji ya makumi kwa maelfu ya watu kuanzia mwaka 1998 hadi mwaka 2000.
Mgogoro uliopo sasa kati yao kulingana na serikali ya Eritrea, ni azma ya Ethiopia isiokuwa na bandari kutaka kuwa na bandari na kujipatia nafasi ya kufikia bahari ya shamu.
Abiy asema Ethiopia haitafuti mzozo na Eritrea
Rais Isaias Afwerki anaeiongoza Eritrea kwa mkono wa chuma tangu ilipojipatia uhuru wake ametoa onyo kwa Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed kwamba nchi yake haitotishika licha ya kuwa na idadi ndogo ya watu.
Ethiopia ina jumla ya watu milioni 130 huku Eritrea inao raia wapatao milioni 3.5.
Afwerki ameonya kwamba Abiy ni lazima asuluhishe matatizo ya kisiasa nchini mwake kabla ya kuwaburuza waethiopia katika vita anavyodai vitamnufaisha Abiy kisiasa.