Rais wa Eritrea aionya Ethiopia dhidi ya kuzua vita vipya
21 Julai 2025Rais Afwerki ambaye ameiongoza Eritrea kwa mkono wa chuma tangu ijitangazie uhuru wake, amemuonya waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed kwamba hawataweza kuwashinda nguvu kwa kuzingatia idadi yao pekee.
Rais wa Eritrea aionya Ethiopia kuhusu kuanzisha vita dhidi yake
Akilihutubia taifa kupitia kituo rasmi cha televisheni, Rais Afwerki alisisitiza kuwa Ethiopia inajidanganya kwa kudhani kuwa idadi ya watu wake ni silaha dhidi yao.
Kwa nini Ethiopia na Eritrea ziko ukingoni kuingia vitani?
Badala yake, Rais Afwerki amesema kabla ya Abiy kulitumbukiza taifa hilo katika vita, ama kutumia raia kwa ajenda nyingine ya kisiasa, Ethiopia inapaswa kusuluhisha kwanza matatizo yake ya ndani.
Pia amevitaja vitendo vya Abiy kuwa juhudi za kiholela za kupuuza matatizo ya ndani.