Rais wa China akataa mwaliko wa EU
16 Machi 2025Rais wa China Xi Jinping amekataa mwaliko wa kushiriki mkutano wa kilele wa maadhimisho ya miaka 50 ya uhusiano wa kidiplomasia wa Ulaya na China mjini Brussels- Ubelgiji. Kwa mujibu wa mtandao wa habari wa Financial Times, China imewaambia maafisa wa Umoja wa Ulaya kuwa Waziri Mkuu Li Qiang atakutana na marais wa Baraza na Tume la Ulaya badala ya rais Xi.
Soma zaidi. Ukraine yazidungua droni 47 zilizorushwa na Urusi
Kwa kawaida Waziri Mkuu wa China ndiye huhudhuria mkutano huo unapokuwa unafanyika mjini Brussels, wakati rais huwa mwenyeji mjini Beijing, lakini Umoja Ulaya ulimtaka Rais Xi kuhudhuria maadhimisho ya nusu karne ya mahusiano baina yao.
Mvutano kati ya Umoja wa Ulaya na China umeongezeka tangu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine mnamo 2022, huku Umoja huo ukiishutumu China kwa kuiunga mkono Urusi. Mwaka uliopita, muungano huo wa Ulaya uliweka ushuru kwa magari ya umeme yanayoagizwa kutoka China.