Rais wa Cameroon Paul Biya atangaza kuwania muhula wa nane
14 Julai 2025Matangazo
Uamuzi huo unamaliza maswali juu ya iwapo angegombea tena nafasi hiyo.
Tangazo la uamuzi huo amelitoa kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X akisema atakuwa mgombea katika uchaguzi wa Oktoba 12 kupitia chama chake cha Cameroon People's Democratic Movement (CPDM) ambacho yeye ni mwenyekiti.
Biya mwenye wa umri miaka 92 ameitawala Cameroon kwa miaka 43 na mnamo miaka ya karibuni hali dhaifu ya afya yake imekuwa chanzo cha mjadala nchini humo.
Washirika wake wawili wa zamani wamejitenga naye na sasa wanawania pia kiti cha urais ikiwemo waziri mkuu wa zamani Bello Bouba Maigari atakayekuwa mgombea wa chama cha NUDP.