SiasaBurundi
Rais wa Burundi awatuhumu maafisa wa umma kulihujumu taifa
31 Julai 2025Matangazo
Rais huyo amesema hilo ni kutokana na kushindwa kwao kuwafichua watu anaoamini kuwa wanapora rasilimali za nchi hiyo.
Ndayishimiye amegusia tatizo la uhaba mkubwa wa mafuta unaotatiza shughuli za Burundi kwa karibu miaka mitatu sasa, pamoja na uhaba wa fedha za kigeni akisema matatizo yote hayo yanasababishwa na watu wasiofichuliwa na maafisa wa umma.
Licha ya rais Ndayishimiye kusifiwa kutokomeza machafuko na umwagaji damu ulioshuhudiwa wakati wa utawala wa mtangulizi wake Pierre Nkurunziza, rekodi ya haki za binadamu bado ni mbaya huku udhibiti wa taifa hilo ukisalia mikononi mwa kundi dogo la majenerali wenye nguvu.