SiasaMarekani
Trump kuanza ziara Jumatatu huko Saudi Arabia, Qatar na UAE
10 Mei 2025Matangazo
Katika ziara hiyo, Trump anatarajiwa kusaini mikataba mikubwa ya kibiashara katika sekta za ulinzi, usafiri wa anga, nishati na akili mnemba.
Ziara ya Trump iliyotajwa na Ikulu ya White House kuwa ya kihistoria, itafanyika chini ya kiwingu cha orodha ndefu ya migogoro katika kanda ya Mashariki ya Kati ikiwa ni pamoja na vita vya Israel huko Gaza, mashambulizi ya Wahouthi wa Yemen, mpango wa nyuklia wa Iran na machafuko nchini Syria nchini ya utawala mpya.
Israel ambayo ni mshirika mkuu wa Marekani eneo hilo kutokuwa kwenye ratiba ya ziara hiyo ya Trump, kumezusha uvumi kuhusu mvutano uliopo kati ya Trump na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kuhusiana na vita vya Gaza.