SiasaMarekani
Rais Trump kuzungumza na Waziri Mkuu wa Japan, Shigeru
7 Februari 2025Matangazo
Viongozi hao wawili wanaotiwa mashaka na kutanuka kwa nguvu za kijeshi na ushawishi wa China wanatazamiwa kutoa tamko la pamoja kuahidi "enzi mpya ya ustawi" kwenye mahusiano ya Japan na Marekani.
Ishiba ambaye anakuwa kiongozi wa pili wa kigeni kumtembelea Trump tangu alipoapishwa karibu wiki tatu zilizopita, anatumai mazungumzo mjini Washington yatamudu kuipeusha nchi yake kuwekewa ushuru ambao Trump ametishia kuziwekea nchi nyingine washirika.
Hadi sasa Trump bado hajaonesha dhamira ya kuzilenga kwa ushuru nchi rafiki kwa Marekani kwenye kanda ya Asia na Pasifiki ikiwemo Japan na Korea Kusini.