Rais Trump kukutana Riyadh na viongozi wa nchi za Ghuba
4 Mei 2025Matangazo
Chanzo kilichopo karibu na serikali ya Saudi Arabia kimetoa taarifa hiyo leo kwa shirika la habari la AFP. Trump atakutana na viongozi wa baraza la ushirikiano la nchi za Ghuba mjini Riyadh kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa kisiasa na kiuchumi kati ya Marekani na nchi hizo.
Soma pia: Mataifa ya ghuba yamejiandaaje baada ya biashara ya mafuta?
Rais huyo wa Marekani anatarajiwa kuzitembelea Saudi Arabia, Falme za Kiarabu, Bahrain, Qatar, Kuwait na Oman kuanzia tarehe 13 hadi16. Kabla ya ziara hiyo, Marekani iliidhinisha siku ya Ijumaa kuiuzia Saudi Arabia makombora ya thamani ya dola bilioni 3.5.