BiasharaMarekani
Rais Trump asaini amri ya ushuru mpya kwa washirika wake
1 Agosti 2025Matangazo
Serikali ya Marekani imesema ushuru huu mpya utaanza kutumika Agosti 7 badala ya siku ya Ijumaa kama alivyoahidi awali.
Hatua hii inaashiria nia ya serikali ya Trump ya kuongeza muda zaidi wa kuoanisha viwango vya ushuru, amesema afisa mwandamizi aliyezungumza na waandishi wa habari kwa sharti la kutotambulishwa.
Agizo hilo linahusisha nchi 68 na Umoja wa Ulaya wenye wanachama 27 uliowekewa ushuru wa asilimia 15. Mataifa ambayo hayajaorodheshwa katika amri hiyo yatawekewa ushuru wa asilimia10.