SiasaMarekani
Rais Trump asaini amri kuidhinisha vikwazo dhidi ya ICC
7 Februari 2025Matangazo
Amri hiyo inasema mahakama ya ICC imetumia vibaya mamlaka yake kwa kutoa waranti za kukamatwa zisizo msingi zinazowalenga waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na waziri wa zamani wa ulinzi Yoav Gallant.
Trump anaituhumu mahakama ya ICC kwa tabia mbaya. Marekani na Israel haziitambui mahakama hiyo. Waranti za kukamatwa Netanyahu na Gallant zilitolewa mwaka uliopita kwa madai ya kufanya uhalifu wa kivita katika vita vya Gaza.
Trump pia anaishutumu mahakama ya ICC kwa kutumia mamlaka yake bila msingi halali na kuanzisha uchunguzi wa awali dhidi ya wafanyakazi wa Marekani.