MigogoroYemen
Rais Trump aonya juu ya kuwaangamiza waasi wa Kihouthi
20 Machi 2025Matangazo
Kituo cha televisheni kinachoongozwa na Wahouthi cha Al-Masirah kimesema mashambulizi hayo yameripotiwa katika mji mkuu Sanaa na eneo la kusini mwa Yemen la Al-Suwaidia katika mkoa wa al-Bayda linalofahamika kama ngome ya kijeshi ya waHouthi.
Rais wa Marekani Donald Trump ametoa onyo kali kwa waasi hao kwamba atawaangamiza.
Soma pia: Marekani, Wahouthi waapa kuendelea kushambuliana
Ameitaka Iran ambayo ndiyo mfadhili wao mkuu, kusitisha uungwaji wake mkono, akisema itawajibika na kukabiliwa na madhara makubwa ikiwa waasi hao watashambulia tena.
Iran imesema Wahouthi wako huru na hujiamulia wenyewe kuhusu maamuzi yao ya kimkakati na kiutendaji.