Rais Samia wa Tanzania achukua fomu ya kugombea Urais
9 Agosti 2025Matangazo
Rais Samia aliambatana na mgombea mwenza Emmanuel Nchimbi wakikiwakilisha chama tawala CCM katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu. Baada ya kuchukua fomu, rais Samia ambaye ndiye Mwenyekiti wa CCM anatarajiwa kuzungumza na wanachama wa CCM.
Hii itakuwa mara ya kwanza kwa Samia kuwania rasmi kiti cha urais nchini Tanzania . Miaka minne iliyopita, akiwa makamu wa rais aliapishwa kuiongoza Tanzania kufatia kifo cha aliyekuwa rais wa wakati huo John Pombe Magufuli.