Rais Putin kukutana na Witkoff mjini Saint Petersburg
11 Aprili 2025Matangazo
Rais wa Urusi Vladimir Putin anatarajiwa kukutana hivi leo na mjumbe maalumu wa Marekani kwa ajili ya mzozo wa Ukraine Steve Witkoff mjini Saint Petersburg.
Witkoff yuko ziaranai nchini Urusi kama sehemu ya jitihada za rais wa Marekani Donald Trump kutaka kuvikifikisha mwisho vita vya Ukraine.
Msemaji wa utawala wa Kremlin Dmitry Peskov amesema ziara ya Witkoff haitakuwa na umuhimu mkubwa na ametahadharisha hakutarajiwi kupatikana makubaliano yoyote makubwa katika mazungumzo kati ya Witkoff na rais Putin kuhusu Ukraine.