Urusi na Uturuki zajadili juhudi za kumaliza vita Ukraine
27 Mei 2025Matangazo
Rais wa Urusi Vladmir Putin na waziri wa mambo ya nje wa Uturuki, wamefanya mazungumzo mjini Moscow kuhusu juhudi za kumaliza vita nchini Ukraine pamoja na hatua zilizopigwa tangu yalipoanzishwa mazungumzo ya moja kwa moja kati ya Urusi na Ukraine.
Vyanzo kutoka wizara ya mambo ya nje ya Uturuki vimesema, waziri Hakan Fidanambaye yuko Moscow kwa ziara ya siku mbili alikutana jana Jumatatu na Putin pamoja na kiongozi wa ujumbe wa Urusi kwenye mazungumzo ya Ukraine, Vladimir Medinsky.
Waziri huyo wa mambo ya nje wa Uturuki anatarajiwa leo kukutana na mwenzake wa Urusi Sergei Lavrov.
Japo hakuna ratiba ya kufanyika mazungumzo yoyote hapo baadae kati ya Urusi na Ukraine,Uturuki imekuwa ikisema inaweza kuwa mwenyeji wa mazungumzo hayo.