Rais Pezeshkian wa Iran aridhia kujiuzulu makamu wake
16 Aprili 2025Rais wa Iran Masoud Pezeshkian, ameidhinisha hatua ya kujiuzulu kwa mmoja wa makamu wake, ambaye alikuwa ni mjumbe muhimu wa Tehran katika mazungumzo yaliyofanikisha kupatikana makubaliano ya Nyuklia ya mwaka 2015 na nchi zenye nguvu.Soma pia: Umoja wa Ulaya: Hakuna mbadala wa diplomasia kuhusu nyuklia ya Iran
Hatua hiyo imekuja wakati Iran inajiandaa kumkaribisha leo Jumatano, mkuu wa shirika la kudhibiti nguvu za Atomiki duniani la IAEA, Rafael Grossi.Soma pia:Iran yasema imeanza mazungumzo yasiyo ya ana kwa ana na Marekani
Aidha kuondoka kwa Mohammad Javad Zarif, kulikotangazwa jana Jumanne, kumekuja chini ya kiwingu cha maandalizi ya duru ya pili ya mazungumzo kati ya Marekani na Tehran kuhusiana na mpango wake wa Nyuklia, yatakayofanyika Roma.